NGUGI WA THIONGO MICERE MUGO: Mzalendo Kimathi
1. Fafanua mbinu za kisanaa ambazo waandishi wa tamthilia Mzalendo Kimathi walitumia na uonyeshe jinsi zilivyochangia katika uwasilishaji wa ujumbe.
2. Kwa kurejelea tamthilia ya Mzalendo Kimathi, eleza madhumuni ya mwandishi kuwatumia wahusika hawa:
a) Mvulana
b) Johnnie
c) Henderson
WILLIAM SHAKESPEARE: Juliasi Kaizari
3. Jadili mbinu za kisanaa ambazo mwandishi wa tamthilia Julia Kaizari ametumia kuwasilisha ujumbe wake kwa wasomaji
4. Tambua sifa za wahusika wafuatao na kasha ufafanue mchango wao katika kuendeleza ploti ya tamthilia, Juliasi Kaizari
a) Juliasi Kaizari
b) Kasio
5. SAID A. MOHAMED: Janga la Werevu
Bamkuu:
Busara: |
Look! (Anasita kwa muda nfupi) tazama ukurasa wa tatu wa gazeti la Mazingira…(anamwambia Bimkuu, mkewe). Hilo ni kosa? Kosa gani? Hilo haliitwi kosa. Linaitwa choyo tu inayotuzushia mkasa huu wa kunyanganywa ardhi zetu. (Amelieleka gazeti analosoma.) Lakini mama watu Maji tunayaharibu sisi, sio wao. Kunywa, kufua tumba za nguo tunazobadiisha kila siku. Kupiga deki nyumba na kumwagia mimea ya maua bustanini. Kuogelea kwenye mabwawa uani… Yale tunayoyaita swimming pools, kwa umaarufu na fanari. Mabwawa ya maji moto na maji bandi. Na kutia mifereji na chemchemi bandia sebuleni. Wao maskini wanatafuta hata tone moja ka maji hawalioati. Kila siku tunasoma kwenye magazeti juu ya tatizo la ukame na mazao kuungua na kukauka. Tunasoma magazetini, na kusikia redioni na kuona kwa macho runingani. Tunaona hata watoto wakinywa ishii ya ng’ombe ili kunusuru uhai wao. Tumeona wanawake wakitafuna magome na kuguguna miti kupata japo mate wameze. |
Maswali:
a) Liweke dondoo hili katika mkutadha wake.
b) Jadili mazingira yanayoonyeshwa katika dondoo hili
ch) Kulingana na dondoo hili, ni nini chanzo cha ukosefu wa manji?
d) Eleza ujumbe unaopatikana katika dondoo hili
e) Changanua mbinu za lugha zinazojitokeza katika dondoo hili.
f) Fafanua sifa za Bimkuu kama zinavyodhihirika katika dondoo
g) Linganisha ujumbe unaopatikana katika dondoo hili na ule unaopatikana katika jamii yako
6. ARI KATINI MWACHOFI: Mama ee
KINAYA:
KINAYA: MWAVITA: |
Nguo zangu mbona si tayari? (kimya) Shemegi ulikuwa ukifanya nini? Mchana kutwa? (kimya) Ee? (kimya.) Jeni aema alikuwa na kazi nyingi, je, wewe ulikuwa ukifanya nini? (kimya. Hasira zampanda kuanza kumtukana Tenge.) Jibu wewe hawara kabla sijakutupa nje ya nyumba yangu na huyo mwanaharamu wako… (Amdakiza kwa hasira) Wacha kumtukana Tenge! Lau una haja sana ya kutukana ntikane mimi maana mimi ndiye nili yemzuia… (Apigwa kofi usoni linalomwangusha chini. Ashika kichwa kwamaumivu. Tenge aanza kupiga mayowe na kumshika na kujaribu kumwinua dadake.) Basi shemegi utamwua. Tangu jana ni mgonjwa hajatia kitu mdomoni wewe wampiga. Mwavita…Mwavita…inuka (Ajaribu kumwinua lakini ashindwa maana ana motto mgongoni. Aketi chini karibu naye huku machozi yatiririka mwavita kimya hajasema kitu. Kinaya atetema kwa hasira afoka na kuzidi kutukana.) Wanawake wawili hapa kazi yao ni kufanya juu chini kuyathakilisha maisha yangu. Leo we Tenge (Amnyoshea kidole.) utatoka nyumbani kwangu na huyo mwanaharamu wako. Sijali uendako mradi tu nisikuone nyumbani kwangu!
|
Maswali:
a) Liweke dondoo hili katika mkutadha wake
b) Fafanua hisia za wahusika wote watatu kulingana na dondoo
ch) Ni fani za lugha zipi ambazo zimetumiwa katika dondoo hili?
d) Jadili maudhui yanayopatikana katika dondoo hili
e) Eleza mafunzo unayoyapata kutoka dondoo hili
f) Linganisha masuala yanayotokea katika dondoo nay ale yapatikanayo katika jamii yako
EBRAHIM HUSSEIN: Kwenye Ukingo wa Thim
7. a) Fafanua migogoro inayojitokeza katika tamthilia, Kwenye Ukingo wa Thim.
b) Eleza mafunzo yanayoweza kupatikana katika tamthilia, Kwenye Ukingo wa Thim.
8.a) Ukitumia mifano mwafaka kutoka tamthilia, Kwenye Ukingo wa Thim, eleza hadhi ya mwanamke
b) Changanua mchango wa Martha Palla katika tamthilia, Kwenye Ukingo wa Thim
JOHN RUGANDA: Mizigo
9. “Mizigo ni anwani mwafaka kwa tamthilia, Mizigo.” Thibitisha ukweli wa kauli hii.
10. a) Kwa kurejelea tamthilia ya Mizigo, dhihirisha kwamba uhusiano mbaya baina ya wazazi wenyeweni balaa kwa familia nzima
b) Matatizo ya kifamilia yaliyomo katika tamthilia ya Mizigo yangeweza kutatuliwa vipi?
BUKHEIT AMANA: Zabibu Chungu
11. a) Jadili hadhi ya mwanamke katika tamthilia, Zabibu Chungu
b) Eleza jinsi mwanamke anavyojitetea katika tamthilia, Zabibu Chungu
12. Mgogoro kati ya ukale na usasa ndilo jambo muhimu ambalo linasisitizwa katika tamthilia, Zabibu Chungu. Jadili kauli hii ukitumia mifano inayofaa kutoka tamthilia yenyewe.
SAID A. MOHAMED: Kivuli Kinaishi
13. a) “Kivuli Kinaishi ni anwani mwafaka ya tamthilia ya Said A Mohamed.” Jadili
b) “Bi Kirembwe ndiye anayestahili kulaumiwa kwa maafa yanayowakumba binadamu wa Giningi.” Thibitisha ukweli wa dai hili ukirejelea tamthilia, Kivuli Kinaishi
14.. a) Eleza dhamira ya mtunzi wa Kivuli Kinaishi
b) Huku ukirejelea tamthilia ya Kivuli Kinaishi, pendekeza mbinu za ujenzi wa jamii bora.