SEHEMU A

WILLIAM SHAKESPEARE: Juliasi Kaizari

1. Jadili mbinu za kisanaa ambazo mwandishi wa tamthilia Julia Kaizari ametumia kuwasilisha ujumbe wake kwa wasomaji

2. Tambua sifa za wahusika wafuatao na kasha ufafanue mchango wao katika kuendeleza ploti ya tamthilia, Juliasi Kaizari

a) Juliasi Kaizari

b) Kasio

NGUGI WA THIONGO MICERE MUGO: Mzalendo Kimathi

3. Fafanua mbinu za kisanaa ambazo waandishi wa tamthilia Mzalendo Kimathi walitumia na uonyeshe jinsi zilivyochangia katika uwasilishaji wa ujumbe.

4. Kwa kurejelea tamthilia ya Mzalendo Kimathi, eleza madhumuni ya mwandishi kuwatumia wahusika hawa:

a) Mvulana

b) Johnnie

c) Henderson

SEHEMU B

SAID A. MOHAMED: Janga la Werevu

Bamkuu:
Bimkuu:


Bamkuu:


Busara:Bimkuu:

 

 

Busara:

Look! (Anasita kwa muda nfupi) tazama ukurasa wa tatu wa gazeti la Mazingira…(anamwambia Bimkuu, mkewe).
Wanasema watachuka ardhi, mashamba na viwanja vyetu vyote vya Msitu wa Uma bilaya fidia. Kosa letu ni lipi lakini? (Akifungua na kupekua gazeti la Mazingira.)

Kwani kuna kosa? Si basi tu. Eti wanasingizia kukatwa miti ndio chanzo cha kukauka maji! Wanasahau kwamba tulifyeka msitu kwa jasho letu na gharama zetu kwa maslahi ya nchi hii. Tukaanzisha mashamba makubwa ya ya chai, pareto na kahawa na kutoa ajira kwa wafanyakazi. Tukazalisha vyakula na mazao ya biashara. Kuna ubaya gani? Kuna ubaya gani kuwaajiri ahwa maskini wasioweza kujilisha wala kujivisha? Kuna ubaya gani kuwahurumia hawa vinyangarika kwa kuwapa ajira?

Hilo ni kosa? Kosa gani? Hilo haliitwi kosa. Linaitwa choyo tu inayotuzushia mkasa huu wa kunyanganywa ardhi zetu.

(Amelieleka gazeti analosoma.) Lakini mama watu
wanasumbuka sana kwa uchache na ukosefu wa maji. Na sisi tunafanya nini? Tunafanya dhambi kubwa. Sikiliza huko nje maji yanavyomwagwa ovyo kwa kuosha magari mengi tuliyo nayo wakati wengine hawana hata tone moja la maji ya kunywa. Pia tumefungua biashara ya maji tunayosomba katika chemchemi za maji za misitu ya wananchi. Na miongoni mwetu hata maji machafu ya sumu tunawauzia watu kuharibu siha zao na kuwaua.

Maji tuliyo nayo ni ya visima tulivyovichimba sisi wenyewe. Na hayo tunayoyatia kwenye magari kuyauza   tunayachukua kutokana na vianzo vya maji vya wananchi kwa sababu na sisi pia ni wananchi. Lakini sisi tuna maji tele kwa sababu tunajua kuya tumia na kuyahifadhi. Wao ndiyo kazi yao   kukwaga maji ovyo na kuyaharibu, si sisi kamwe!

Maji tunayaharibu sisi, sio wao. Kunywa, kufua tumba za nguo tunazobadiisha kila siku. Kupiga deki nyumba na kumwagia mimea ya maua bustanini. Kuogelea kwenye mabwawa uani… Yale tunayoyaita swimming pools, kwa umaarufu na fanari. Mabwawa ya maji moto na maji bandi. Na kutia mifereji na chemchemi bandia sebuleni. Wao maskini wanatafuta hata tone moja ka maji hawalioati. Kila siku tunasoma kwenye magazeti juu ya tatizo la ukame na mazao kuungua na kukauka. Tunasoma magazetini, na kusikia redioni na kuona kwa macho runingani. Tunaona hata watoto wakinywa ishii ya ng’ombe ili kunusuru uhai wao.   Tumeona wanawake wakitafuna magome na kuguguna miti kupata japo mate wameze.

 

Maswali:

a) Liweke dondoo hili katika mkutadha wake.

b) Jadili mazingira yanayoonyeshwa katika dondoo hili

ch) Kulingana na dondoo hili, ni nini chanzo cha ukosefu wa manji?

d) Eleza ujumbe unaopatikana katika dondoo hili

e) Changanua mbinu za lugha zinazojitokeza katika dondoo hili.

f) Fafanua sifa za Bimkuu kama zinavyodhihirika katika dondoo

g) Linganisha ujumbe unaopatikana katika dondoo hili na ule unaopatikana katika jamii yako

 

ARI KATINI MWACHOFI: Mama ee

KINAYA:

MWAVITA:

  


TENGE:
 

 

 

KINAYA:

 

MWAVITA:

Nguo zangu mbona si tayari? (kimya) Shemegi ulikuwa ukifanya nini? Mchana kutwa? (kimya) Ee? (kimya.) Jeni aema alikuwa na kazi nyingi, je, wewe ulikuwa ukifanya nini? (kimya. Hasira zampanda kuanza kumtukana Tenge.) Jibu wewe hawara kabla sijakutupa nje ya nyumba yangu na huyo mwanaharamu wako…

(Amdakiza kwa hasira) Wacha kumtukana Tenge! Lau una haja sana ya kutukana ntikane mimi maana mimi ndiye nili yemzuia… (Apigwa kofi usoni linalomwangusha chini. Ashika kichwa kwamaumivu. Tenge aanza kupiga mayowe na kumshika na kujaribu kumwinua dadake.)

Basi shemegi utamwua. Tangu jana ni mgonjwa hajatia kitu mdomoni wewe wampiga. Mwavita…Mwavita…inuka (Ajaribu kumwinua lakini ashindwa maana ana motto mgongoni. Aketi chini karibu naye huku machozi yatiririka mwavita kimya hajasema kitu. Kinaya atetema kwa hasira afoka na kuzidi kutukana.)

Wanawake wawili hapa kazi yao ni kufanya juu chini kuyathakilisha maisha yangu. Leo we Tenge (Amnyoshea kidole.) utatoka nyumbani kwangu na huyo mwanaharamu wako. Sijali uendako mradi tu nisikuone nyumbani kwangu!


(Aketi afuta machozi na kumwangalia Kinaya) Wanawake wawili hao uliwaoa wewe wote? Huna haya kumtukana shemegi yako kama mkeo? Sikubali unitukane mimi na dadangu pia!

 

Maswali:

a) Liweke dondoo hili katika mkutadha wake

b) Fafanua hisia za wahusika wote watatu kulingana na dondoo

ch) Ni fani za lugha zipi ambazo zimetumiwa katika dondoo hili?

d) Jadili maudhui yanayopatikana katika dondoo hili

e) Eleza mafunzo unayoyapata kutoka dondoo hili

f) Linganisha masuala yanayotokea katika dondoo nay ale yapatikanayo katika jamii yako

 

SEHEMU CH

SAID A. MOHAMED: Kivuli Kinaishi

7. a) “Kivuli Kinaishi ni anwani mwafaka ya tamthilia ya Said A Mohamed.” Jadili

b) “Bi Kirembwe ndiye anayestahili kulaumiwa kwa maafa yanayowakumba binadamu wa Giningi.” Thibitisha ukweli wa dai hili ukirejelea tamthilia, Kivuli Kinaishi

8. a) Eleza dhamira ya mtunzi wa Kivuli Kinaishi

b) Huku ukirejelea tamthilia ya Kivuli Kinaishi, pendekeza mbinu za ujenzi wa jamii bora.

JOHN RUGANDA: Mizigo

9. “Mizigo ni anwani mwafaka kwa tamthilia, Mizigo.” Thibitisha ukweli wa kauli hii.

10. a) Kwa kurejelea tamthilia ya Mizigo, dhihirisha kwamba uhusiano mbaya baina ya wazazi wenyeweni balaa kwa familia nzima

b) Matatizo ya kifamilia yaliyomo katika tamthilia ya Mizigo yangeweza kutatuliwa vipi?

SEHEMU D

EBRAHIM HUSSEIN: Kwenye Ukingo wa Thim

11. a) Fafanua migogoro inayojitokeza katika tamthilia, Kwenye Ukingo wa Thim.

b) Eleza mafunzo yanayoweza kupatikana katika tamthilia, Kwenye Ukingo wa Thim.

12.a) Ukitumia mifano mwafaka kutoka tamthilia, Kwenye Ukingo wa Thim, eleza hadhi ya mwanamke

b) Changanua mchango wa Martha Palla katika tamthilia, Kwenye Ukingo wa Thim

 

BUKHEIT AMANA: Zabibu Chungu

13. a) Jadili hadhi ya mwanamke katika tamthilia, Zabibu Chungu

b) Eleza jinsi mwanamke anavyojitetea katika tamthilia, Zabibu Chungu

14. Mgogoro kati ya ukale na usasa ndilo jambo muhimu ambalo linasisitizwa katika tamthilia, Zabibu Chungu. Jadili kauli hii ukitumia mifano inayofaa kutoka tamthilia yenyewe.

MWISHO